Safarilands.org

Buriani ahimiza utunzaji wa mazingira
By Zaina Malongo

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk. Batirida Buriani amewataka wananchi kuzingatia usafi wa mazingira kwa kutotupa taka ovyo ili kutunza mazingira kwa wakati wote.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk. Batirida Buriani amewataka wananchi kuzingatia usafi wa mazingira kwa kutotupa taka ovyo ili kutunza mazingira kwa wakati wote.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira barani Afrika iliyofanyika katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo, jijini Dar es Salaam, Buriani alisema wito wake kwa kila Mwananchi kutunza na kulinda mazingira ili nayo yamtunze na kwamba hilo si jukumu la Serikali peke yake.

Alisisitiza kuwa kila mmoja ni mlinzi wa mazingira na kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo isemayo "Epuka utupaji taka ovyo, kwa ajili ya kutunza mazingira kwa jamii nchi si kwa mtu mmoja mmoja."

"Ikiwa kila mmoja ataweza kutunza mazingira, hata wageni watakaotembelea nchi yetu kwa ajili ya kufanya utalii watavutiwa na jinsi watakavyokuta mazingiwa yetu masafi, kwa kuwa tumeyatunza katika hali nzuri," alisema Buriani.

Akitoa mfano wa Jiji la Mwanza alisema jiji hilo kuwa limendelea kwa kutunza mazingira na kwamba inawezekana kwa miji mingine kuiga mfano wake kwa kutembelea Mwanza na kujifunza ulipoanzia.

Naye Mkurungenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Mazingira (NEMC) Dk,Robert Ntakamulenga alisema tangu mwaka 2000 sheria ya utoaji elimu ya mazingira kwa ajamii nzima ilipotungwa serikali ilipanga siku maalumu ya kuadhimisha utunzaji wa mazingira kwa kufanya vitendo mbalimbali kuonyesha jamii inayotuzunguka.

"Hivyo Baraza la Taifa limeweza kuweka watendaji kazi kwa kuzunguka kila maeneo kila baada ya siku tano kwa kupitia kuangalia hali ya mazingira na usafi inaendeleaje kwa ujumla ndani ya hizo siku mfululizo," alisema Ntakamulenga.

Aliongeza ni jukumu la kila mmoja kutunza mazingira kama sheria ya mwaka 2000 inavyosema na yeyote atakayepingana nayo hatua dhidi yake zitachukuliwa ikiwemo kifungo cha miezi mitatu hadi saba au kutozwa faini kati ya Sh50,000 hadi Sh1,000,000.
Copyright © 2005, Safarilands.org