|
|
|||||||||
|
Join mailing list
Use Email to Register
|
Tourism
Biashara ya utalii na maadili yake - Zanzibar
Posted: Monday February 11, 2008 5:52 PM BT
![]() The Vision of the Government of Zanzibar regarding tourism is "To become one of the top tourism destinations of the Indian Ocean, offering an up market."
> Haikuwa sekta ya biashara bali ni kujifurahisha tu, > Kutokana na maendeleo katika sekta ya mawasiliano, kukua kwa uchumi katika nchi zilizoendelea pamoja kubadilika kwa sheria za kazi sekta ya utalii ilipata msukumo na sura mpya. > Katika miaka ya themanini (80) sekta ya utalii ilianza kuwa moja kati ya zinazochanguliwa kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi. Nani mtalii na nini utalii? > Mtalii ni mtu anayesafiri kutoka eneo moja (makazi yake ya kawaida)kwenda sehemu nyengine kwa ajili ya kutembea, kupumzika (kustarehe), matibabu, masomo na biashara, > Utalii ni kitendo cha mtu kusafiri nje ya makazi yake ya kawaida kwa lengo la kutembea, kupumzika (kustarehe), matibabu, masomo na biashara. > Biashara ya utalii hujumuisha safari yote ya mtalii tokea sehemu yake ya makazi hadi sehemu anayeitembelea. Hali ya utalii - Zanzibar > Mwaka 1985 Zanzibar ilipokea watalii 19,368. Mwaka 1990 tulipokua watalii 42,141. Mwaka 2000 tulipata watalli 97,165. Mwaka 2005 watalii walizidi na kufikia 125,443 na mwaka uliopita. 2006 watalii na kufikia 137,111 ukilinganisha takwimu hizi idadi ya watalii inaongezeka kwa kasi. > Idadi ya nyumba za kulala watalii zimeongezeka kufikia 234 mwaka 2007, maduka ya zawadi za kitalii yameongezeka 120, huduma za usaflrishaji zimeimarika, taasisi za kutembeza wageni nazo zimeongezeka 215. > Mahitaji ya bidhaa kama vile matunda, samaki, nyama na vyakula vyengine yameongezeka kutokana na ongezeko la watalii. Malengo ya utalii Malengo Makuu ya sekta ya Utalii ni:- > Kuingizia serikail fedha za kigeni > Kuongeza nafasi za ajira > Kupanua wigo wa uchumi > Kukuza sekta nyengine za Uchumi > Kuhifadhi mali asili > Kuboresha huduma za jamii Kwa mujibu wa sheria Nambari 9 ya mwaka 1996 maana ya biashara ya utalii ni biashara yeyote ile inayotoa huduma kwa mtalii ikijumuisha Mikahawa, kumbi za Dansi na Disco, Hoteli za kitalii, Nyumba za kulaza wageni, * Makampuni ya kutembeza wageni, Maduka ya zawadi kwa wageni, ukodishaji wa magari kwa wageni, Mapikipiki, Baiskeli, usafiri wa barabara na Anga, michezo ya baharini pamoja na huduma yeyote yenye maumbile ya kutoa huduma kwa mtalii. Biashara ya kutoa huduma hizo inayotolewa na Karnisheni ya Utalii. Kwa mujibu wa kifungu nambari 8 (3) Kamisheni ya Utalii haina uwezo wa moja kwa moja kutoa leseni kwa mfanyabiashara yeyote wa utalii hadi atakapothibitisha kulipa kodi na kuonyesha stakabadhi hiyo. Kero katika maeneo ya biashara ya utalii Kwa vile biashara hii ni ya kutoa huduma kwa watalii tokea kuanza na kukua kwa biashara hii kumejitokeza wimbi kubwa la makero yanayovunja kwa njia moja au nyengine maadili ya biashara ya utalii. Kero katika kiwanja cha ndege na bandarini > Kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaoomba fedha aii hata kudai rushwa katika kiwanja cha ndege. > Wengi wanaofanya hivyo ni maafisa wa Serikali kutoka katika taasisi mbali mbali likiwemo Jeshi la Polisi. > Aidha kumekuwa na ongezeko kubwa la wafanyabiashara za mikononi, watoto na wazee wanaomba omba pamoja watembezaji wenye makampuni hewa kusubiri wageni katika maeneo ya kiwanja. > Mali hii haikubaliki na haitoi taswira njema kwa wageni wanaoitembelea Zanzibar. > Kwa upande wa Bandarini ambapo wageni wanaotoka Dar es Salaam hukumbana na mazingira ambayo hayaendani na maadili ya sekta ya utalii. > Wageni hao wanapotoka nje ya lango la bandari hufuatwa na makundi ya vijana na kulazimishwa kufuatana nao. > Vijana hao hawana uhalali wa kufanya kazi hiyo na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi yao. Kero ndani ya Mji Mkongwe > Wageni wengi wanaokuja Zanzibar hupenda kutembetea Mji Mkongwe kutokana na uzuri wa haiba yake na historia. > Katika Mji Mkongwe kuna maeneo yanayoruhusiwa kupitisha magari na mengine hayaruhusiwi. Hali illvyo sasa ni tofauti na utaratibu wa utumiaji wa barabara ulivyowekwa. > Ndani ya Mji Mkongwe kumekuwa na baa za kienyeji, kumbi za starehe zisizokubalika n.k. > Biashara hizi zisizokuwa halali zimekuwa ni kero kwa wananchi wa maeneo hayo na zinapotosha maadili na utamaduni wa wazanzibar. > Kumekuwa na ongezeko kubwa na watu waryaojuhusisha na biashara ya ukahaba ndani ya maeneo ya Mji Mkongwe. > Bado hatua za kuthibiti hali hii kwa vyombo husika sio za kurithisha. Kero katika fukwe za mahoteli (beach boy's) > Hapa Zanzibar mahoteli mengi yapo katika fukwe. > Wageni wengi hupenda kupumzika kwenye fukwe au kuogelea baharini. > Kwa sasa maeneo hayo yamekuwa ni maeneo ya biashara za mikononi na na nyengine zisizokuwa halali. > Biashara hizi haziruhusiwi kufanywa katika maeneo hayo. Kero kwa Askari Polisi Kusimamisha Magari, Kudadisi na Kuomba > Zanzibar kijiografia iko mbali. > Wageni wengi wanaosafiri kutoka nchi za mbali inawachukua muda mrefu kufika Zanzibar. Hivyo mgeni yeyote anayewasili Zanzibar kwa kiasi anakuwa amechoka na anahitaji kufikishwa Hotelini kwa usalama na kwa haraka iwezekanavyo Hivyo kitendo cha kusimamishwa na kudadisiwa kwa muda mrefu kila baada ya kilomita chache kinampa picha ya kuwa Zanzibar sio salama na watu wake sio waadiiifu. Kwani mgeni huyu huona au hutaka kujua nini kimetokea na nini kimefanyika. Hivyo kila kinachoendelea hutaka kujua. Kwa mujibu wa taarifa za wageni wengi waliondoka kwa njia ya Bandari na Anga wamelalamikia tabia na lugha za Polisi wanapokuwa katika doria za kazi hizo. Hivyo Jeshi la Polisi linapaswa libadilike katika kudadisi na kupekuwa vyombo vya moto. Aidha ni vyema mgeni akajuilishwa kama kuna kasoro zozote zilizojitokeza. Uwezo wa Kisheria wa Kamisheni ya Utalii > Kutoa leseni au kufuta leseni za biashara ya utalii. > Kamisheni ya Utalii inauwezo wa kufuta leseni au kusitisha kutokufanya kazi leseni hiyo kwa muda. > Kamisheni itafuta leseni kwa mtu yeyote atakayevunja masharti ya leseni hiyo, kukiuka au kuvunja kifungu chochote cha sheria ya utalii au sheria yoyote ya nchi. > Kamisheni itafuta leseni kwa mtu yeyote atakae toa taarifa zisizo za kweli au itakapogundulika mfanyabiashara huyo anakwenda kinyume na maadili ya biashara na maadili ya jarnii kwa jumla. > Mfanyabiashara yeyote wa hoteli au nyumba za kulaza wageni mwenye leseni ya biashara hiyo haruhusiwi kufanya kazi ya kuternbeza wageni. > Biashara ya kutembeza wageni ni kwa makampuni ya Wazanzibari tu. > Kwa mujibu wa kifungu Nambari 29 (1) cha Nambari 9 ya mwaka 1996, Kamisheni inauwezo wa kuzuwiya gari lolote la kuternbeza wageni lisilo na leseni au ruhusa halali. > Kufunga biashara yeyote ya utalii kama vile Maduka, Mabaa, Mikahawa na hoteli za kitalii. > Kwa mujibu wa sheria ndogo wa utalii Nambari 46 (1,2,3,4 na 5) mtu yeyote anayetembeza wageni anatakiwa awe na ruhusa au kitambulisho kinachotolewa na Kamisheni ya Utalii. > Aidha kifungu Nambari 84 kinatoa mamlaka kwa Aftsa wa Kamisheni ya Utalii na Askari Polisi kumkamata na kumchukulia sheria mtu yeyote au taasisi yeyote inayofanya biashara kinyume cha sheria |
Advertising
Sponsors Links
Advertising
|
|||||||
|
|||||||||
| Copyright © 2005 Safarilands.org All Rights Reserved. | |||||||||