Safarilands.org
Jamii ya Wasangu Tanzania
URL: https://www.safarilands.org/index.php/people_culture/more/jamii_ya_wasangu_tanzania/
Posted: Thursday July 09, 2009 9:09 AM BT
Posted: Thursday July 09, 2009 9:09 AM BT
Makala haya yanazungumzia habari za Wasangu waishio katika bonde la Usangu katika Wilaya ya Mbeya. Kama inavyojulikana Utafiti huu, ambao unaendelea, wafanywa kwa shida nyingi za usafiri kutoka mahali fulani hadi pengine ambapo utafiti watakiwa ufanyike.
Makala haya yanazungumzia habari za Wasangu waishio katika bonde la Usangu katika Wilaya ya Mbeya. Kama inavyojulikana Utafiti huu, ambao unaendelea, wafanywa kwa shida nyingi za usafiri kutoka mahali fulani hadi pengine ambapo utafiti watakiwa ufanyike. Magari hatuna ambayo yangalituwezesha kufika mahali pa utafiti kwa urahisi zaidi. Safari zotezafanywa kwa miguu na watu ambao pengine wangesaidia kutoa habari wanashindwa kutembea au sisi wenyewe watafiti tunashindwa kuwafikia kwa wakati unaofaa.Zaidi ya hayo, habari nyingi zimesahauliwa sana kwa sababu hakuna mtu aliyejishughulisha kuzitafuta na kuzihifadhi kwa sababu Wazungu walipofika huku kwetu waliziita hizo habari ni za kishenzi. Basi watu wakaziacha na habari zake zikapotea kabisa.
Read More:
Jamii ya Wasangu Tanzania
Copyright © 2005, Safarilands.org